By alanus
MSHAMBULIAJI
Alvaro Morata amekatisha fungate lake Ibiza ili akashughulikie uhamisho
wake kwenda Manchester United kwa mujibu wa gazeti la AS la Hispania.
AS
limeripoti kwamba Real Madrid amesafiri kutoka Ibiza kwenda nyumbani
kwake mjini Madrid, huku mazungumzo ya uhamisho baina ya klabu hizo
mbili yakiendelea.
Morata
amezungumza mara kadhaa kwa simu na kocha wa United, Jose Mourinho na
imeripotiwa yuko njiani kuhamia Ligi Kuu ya Engla
Kocha
wa United, Mourinho amekuwa shabiki wa Morata tangu anamfundisha katika
kipindi chake cha kufanya kazi kwa miaka mitatu Bernabeu.
Mashetani
Wekundu 'walitupa ndoana' zao kwa Morata mwezi uliopita, lakini Madrid
inataka ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 70 kumuuza mchezaji huyo wa
kimataifa wa Hispania.
Mourinho anasaka mshambuliaji mpya Man United kwa sababu Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka siku si nyingi zijazo.
Awali
United walimtaka sana Antoine Griezmann, lakini Mfaransa huyo akaamua
kusaini mkataba mpya Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufungiwa
kusajili.
Mashetani
hao Wekundu walimtaka pia mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku lakini
bahati mbaya mchezaji hiyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameamua kurejea
timu yake ya zamani, Chelsea.
0 comments:
Post a Comment