Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana
Julai 8, mwaka huu pamoja na mambo mengine pia ilijadili mchakato wa
chaguzi za Mkoa wa Rukwa (RUREFA) na timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi
Kuu ya Vodacom.
Kuhusu mchakato wa uchaguzi Mkoa
wa Rukwa (RUREFA), Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Msomi
Wakili Revocatus Kuuli, imeagiza zoezi hilo liendelee na inamtuma Mjumbe
wake siku ya usaili, Msomi Wakili Thadeus Karua kwa ajili ya
kushuhudia.
“Na pia Kamati ya Uchaguzi
itawatuma wajumbe siku ya uchaguzi tarehe 5 Agosti, 2017,” imesema
kamati hiyo ilipoagiza kuhusu kuendelea kwa uchaguzi huo.
Kuhusu uchaguzi wa Lipuli,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Msomi Wakili Kuuli, imemwagiza Katibu
Mkuu wa klabu hiyo, kuendelea na maandalizi ya uchaguzi kama
ilivyoelekezwa na kamati kwamba ufanyike Agosti 5, mwaka huu.
“Na Kamati inamtuma mjumbe wa
Kamati ya Uchaguzi Msomi Wakili Mohamed Ally Mchungahela kwa ajili ya
uangalizi siku ya uchaguzi,” imesema sehemu ya taarifa ya kamati kwa
uongozi wa Lipuli.
Kamati imesisitiza, “Na wanachama waendelee kulipia ada za uanachama kwa kuwa watakaoruhusiwa kupiga kura ni wanachama hai tu.”
0 comments:
Post a Comment