Sakata la usajili wa mchezaji Neymar kwenda Paris Saint
Germain linazidi kushika hatamu.Taarifa mpya zinasema mbinu walizotumia
FC Barcelona kumpata Neymar wakati akiwa mchezaji wa Santos ndio huenda
zikamuondoa Neymar Camp Nou.
Wakati FC Barcelona walipokuwa wakiwinda saini ya Neymar walilipa
kiasi cha 40 million euros kwa baba mzazi wa Neymar kupitia kampuni yake
ya DIS. Malipo haya mwanzoni yaliripotiwa kuwa mkopo lakini baadae
jambo hili lilipelekea kuwepo kwa kesi mahakamani na ikafahamika haikuwa
mkopo, bali kifuta jasho cha kufanikisha mwanae haendi kujiunga na
Madrid bali Barcelona- wakati tayari Neymar alikuwa ameshafanya vipimo
vya afya na alikuwa akikaribia kujiunga na Real Madrid. Vilabu vyote
viwili vilikuwa vimekubali kulipa ada ya uhamisho iliyotakiwa na Santos.
Miaka 3 baadae, akielekea msimu wake wa 4 na FC Barcelona, miamba ya
soka ya Ufaransa Paris Saint Germain wanataka kumsaini Neymar kutoka FC
Barcelona. Miamba hiyo yenye misuli ya pesa wapo tayari kutumia zaidi
ya trillioni 1 za kitanzania kufanikisha uhamisho huo wa nahodha huyo wa
timu ya taifa ya Brazil.
Mwanzoni
taarifa hizi zilipoanza kutoka , watu wengi tuliamini PSG wasingeweza
kuvunja rekodi ya dunia kwa kulipa kiasi cha £197m ili kumsaini,
kwasababu wangekuwa wametoka nje ya sheria ya Financial Fair Play na
hata juzi Rais wa Barca, Josep Bartomeu alikaririwa akisema haamini kama
kuna klabu itaweza kumsaini Neymar kwa kuvunja mkataba wake kwa maana
ya kulipa kiasi hicho cha pesa.
Leo ripoti mpya za usajili wa Neymar zinaeleza kwamba mchezaji huyo
kupitia baba yake tayari amekutana na PSG na kukubaliana vipengele
binafsi na tayari Neymar ameshawaambia baadhi ya wachezaji wenzake
kwamba anaondoka Camp Nou.
Swali PSG watafanikishaje uhamisho huu bila kuvunja sheria ya Financial Fair Play? .
Jibu: Ili PSG waweze kukamilisha uhamisho huo bila kukabiliana
na adhabu za Financial Fair Play, wamiliki wa PSG, serikali ya kifalme
la QATAR
wanaripotiwa kumpa Neymar Dos Santos mkataba wa kuitangaza michuano ya
kombe la dunia 2022 itakayofanyika nchini humo kwa mkataba wenye thamani
ya €222m. Neymar atatumia fedha hizo kulipa fedha za kuuvunja mkataba
wake na FC Barcelona wenye thamani sawa na fedha atakazopewa kwenye dili
la kuitangaza michuano ya World Cup 2022. Baada ya kukamilisha usajili
huo, Neymar anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka wenye thamani ya €150m.
PSG pia watatumia kiasi cha €156m kwa ajili ya kodi. Kwahiyo uhamisho
huu utagharimu jumla ya €528m – zaidi ya trillioni 1 za kitanzania.
0 comments:
Post a Comment