Baada
ya timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza, Kocha
Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania, ameibuka na kusema
kuwa huo ni mwanzo mzuri wa kikosi chake na atahakikisha anauendeleza.
Azam
wakiwa ugenini mkoani Mtwara, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao
1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya wenyeji wao, Ndanda FC.
Kocha
huyo amesema: “Jambo la kushukuru ni kwamba tumeanza vizuri ligi na
kushinda pointi tatu tukiwa ugenini, suala hilo linanipa matumaini
makubwa ya kwamba tunaweza kufanya vizuri sana kwenye msimu huu.
“Hiki
tulichokifanya leo (juzi) nitahakikisha kinaendelea na tunapata matokeo
mazuri kwenye mechi zetu zinazokuja, bila ya kuangalia ni aina gani ya
mpinzani ambaye tutakutana naye.”

0 comments:
Post a Comment