Kiungo mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi kwa sasa hafikirii habari za ufungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara licha ya kufunga magoli manne kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.
Okwi amesema achoangalia kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye kila mechi na kuisaidia timu yake kupata pointi tatu.
“Nataka kuhakikisha kila game nafanya vizuri na kuisaidia timu yangu kwa hiyo sasa hivi siwezi kuwaza mambo ya ufungaji bora ikiwa ndio tumecheza mechi ya kwanza,” Emanuel Okwi.
0 comments:
Post a Comment