Sakata la kiungo wa Yanga SC
aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbao FC Pius Buswita kufungiwa mwaka
mmoja kucheza mpira lapata sura mpya baada ya katibu mkuu wa Yanga ndugu
Charles Boniface Mkwasa kulitolea ufafanuzi.
Buswita amekumbana na rungu la TFF
la kutojihusisha na soka kwa mwaka mmoja baada ya kile kinachodaiwa
kusajili vilabu viwili kwa wakati mmoja yaani Yanga SC na Simba SC .
Simba ndio waliomwekea pingamizi TFF ikidaiwa kawatapeli hivyo kufungiwa
mwaka mmoja.
Mkwasa asubuhi ya leo akiongea na
kituo cha redio ya EFM amekiri kupokea barua ya hukumu hiyo ikiwaeleza
hawataweza kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja kama adhabu yake .
Mkwasa amesema kama klabu pia wameiandikia TFF barua kupinga uamuzi huo
na kulieleza jambo hilo kwa kina sambamba na maelezo ya mchezaji husika .
” Simba SC wanasema Pius
wamemsajili tarehe 2 juni 2017 ilihali kipindi hicho alikuwa ndani ya
mkataba na Mbao FC kitu ambacho ni makosa kwa sababu hawakuwafuata Mbao .
Sisi tumewafuata Mbao na mchezaji husika na tukamsajili , wakatupa
stakabadhi zetu pia release letter kama viambatanisho . Sasa hao Simba
walimsajili Pius yupi? ilihali mkataba wake na Mbao umekwisha tarehe 7
August?! Hii ina maana kwanza kabisa Simba ndio wana makosa katika hili
kumsajili mchezaji wa watu akiwa ndani ya mkataba bila kuonana na
waajili wake. Katika hili Mbao ndio wana haki kuwashitaki Simba ”
alieleza Mkwasa.
Mkwasa kaenda mbali kwa kusema
waliokuwa wakimrubuni kijana huyu kwa milioni 5 kupitia wazazi wake ni
wapenzi wa Simba Mwanza ambao dhamira yao ilikuwa ni kuvuruga usajili
huu hivyo TFF walitakiwa kusikiliza pande zote kabla ya kutoa hukumu (
natural justice ) kuliko walivyofanya.
” sisi na Azam tuligongana kwa
Hozza wa Mbao lakini mwisho wa siku tukaona isiwe tabu kwa sababu
mchezaji husika kaonesha mapenzi ya kwenda Azam , tulipewa pesa zetu na
kuliacha suala hilo bila ugomvi , kwanini Simba ?! ” aling’aka Mkwasa.
Sakata hili kuna kila dalili ya
taratibu za kiusajili kukiukwa pia hukumu kutoka bila kusikiliza kwa
kina pande zote . Hali ambayo imewapelekea Yanga na mchezaji husika
kukata rufaa TFF kwa hukumu waliyotoa.
Wakati huohuo;
Afisa habari wa Simba SC ameeleza suala la mchezaji huyo wanaweza kulipeleka katika mahakama za kiraia kwa kesi ya utapeli.
Afisa habari wa Simba SC ameeleza suala la mchezaji huyo wanaweza kulipeleka katika mahakama za kiraia kwa kesi ya utapeli.
0 comments:
Post a Comment