Thursday, October 26, 2017

Nyota Mbrazil, Willian akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la pili dakika ya pili ya muda wa ziada baada ya kutimia 90 za kawaida katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Kombe la Carabao usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London. Bao lingine la Chelsea lilifungwa na Antonio Rudiger dakika ya 26, wakati la Everton lilifungwa na Dominic Calvert-Lewin dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90. Chelsea inaungana na Manchester United, Manchester City na Arsenal kwenda robo fainali ya michuano hiyo

Usiku wa Jumatano October 25, 2017 nahodha wa Tanzania na klabu ya Genk ya Ubelgiji alifunga bao moja wakati timu yake ikipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Club Brugge kwenye uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena.
Samatta amefunga goli lake dakika ya 90 na kumaliza wimbi la kucheza bila kufunga ambapo alishacheza mechi tisa bila kutupia kabambani kabla ya kuwafunga Brugge, bao la kwanza la Genk limefungwa na Ruslan Malinovskiy dakika ya 43 kipindi cha kwanza.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Genk katika mechi tano zilizopita, kabla ya ushindi huo waliwafunga Anderlecht 1-0 ugenini.
Matokeo ya Genk katika mechi tano zilizopita
  • Genk 1-1 KV Oostende
  • AS Eupen 3-3 Genk
  • Genk 1-1 Royal Excel Mouscron
  • Anderlecht 0-1 Genk
  • Genk 2-0 Club Brugge

0 comments:

Post a Comment