Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema, yalifanyika makosa kwa uongozi wa klabu yake kuwaachia Ibrahim Ajib pamoja na Amis Tambwe ambao wote walisajiliwa Yanga kwa nyakati tofauti.
“Lazima nikiri kwamba viongozi wangu walifanya makosa kumwachia Ajib, ni kijana mzuri lazima niseme ukweli, inawezekana alikuwa na matatizo yake lakini wachezaji hawakosi kuwa na matatizo, kinachotakiwa siku zote ukiwa kiongozi ni kuwa mvumilivu na kujaribu kuwa na lugha nzuri ya kumvuti mchezaji”-Rage.
“Mchezaji mdogo kama Ajib kumuachia au Tambwe ilikuwa ni makosa makubwa kwenye klabu ya Simba. Kwa kuwa ameondoka na kwenda kwa watu, siku zote watu ambao wanatoka Simba kwenda Yanga basi tena wanapoteza ile thamani yao hata uwe mzuri kiasi gani.”
Ajib amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu ya Yanga tangu asajiliwe kabla ya kuanza kwa msimu huu na tayari ameshafunga magoli matano katika mechi saba za VPL. Tambwe pia ameendea kufanya vyema tangu ajiunge na Yanga baada ya kutemwa Msimbazi na amekuwa akiwafunga kwenye mchezo wa watani wa jadi.
0 comments:
Post a Comment