Mafundi wa soka wanazidi tu kutundika daluga, tayari tumeshuhudia mwaka huu wachezaji nyota akiwemo Pirlo, Ricardo Kaka na Xabi Alonso wakiachana na soka, sasa nyota wa zamani wa Barcelona naye anatundika daluga.
Ni Xavi Hernandez ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya Quatar ya Al Sadd. Xavi ametangaza rasmi ya kwamba baada ya msimu huu kuisha baasi atatundika daluga zake na kuamua kuanza kuangalia maisha mengine.
Xavi tangu ameanza kucheza soka ameshcheza jumla ya michezo 890 ambapo katika michezo hiyo amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 103 huku akibeba makombe 8 ya ligi ya nchini Hispania La Liga.
Akiwa na Barcelona kiungo huyo amefanikiwa kushinda michuano ya Champions League mara 4, akashinda michuano ya Copa Del Rey mara 3 huku akiisaidia Hispania kubeba michuano ya Euro mara 1 na kombe la dunia mara 1.
Xavi amesema baada ya kuacha kucheza soka atakaa pembeni na kuanza kuwa kocha kwani mwakani anataraji kupata leseni yake ya ukocha huku akimshukuru mungu kwa kucheza soka kwa muda mrefu bila majeruhi makubwa.
0 comments:
Post a Comment