KLABU ya Manchester City imemsainisha mkataba mpya wa miaka mitano na nusu mchezaji wake nyota, Kevin De Bruyne.
Nyota wa Manchester City, Kevin De Bruyne akisaini mkataba mpya akiwa na mkewe, Michele PICHA ZAIDI GONGA HAPA
De
Bruyne alikubali kusaini wiki iliyopita kwa mshahara wa Pauni 280,000
kwa wiki, ambao utamfanya awe anapokea na posho ya Pauni 70,000.
Na
hii inazima kabisa uwezekano wa mchezaji huyo kwenda Real Madrid na
Barcelona zilizokuwa zinamhitaji pia kutokana na City kumtia pingu za
miguu haraka hadi mwaka 2023.
Na habari njema zaidi kwa kocha Mspaniola, Pep Guardiola ni kwamba kiungo Mbrazil, Fred mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kujiunga na City kutoka Shakhtar Donetsk.
Na habari njema zaidi kwa kocha Mspaniola, Pep Guardiola ni kwamba kiungo Mbrazil, Fred mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kujiunga na City kutoka Shakhtar Donetsk.
De
Bruyne ametulia Jijini Manchester na mkewe, Michele na mwanawe wa kiume
mdogo, Mason na anataka kumfanyia kazi nzuri Guardiola katika miaka
hiyo karibu mitano.
De
Bruyne amefunga mabao 31 katika mechi 122 na kutoa pasi za mabao 50
tangu ajiunge na City kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 55 kutoka
Wolfsburg Agosti mwaka 2015.
De Bruyne anakuwa mchezaji wa tatu wa City kusaini mkataba mpya tangu wiki iliyopita baada ya Nicolas Otamendi na Fernandinho.
De Bruyne anakuwa mchezaji wa tatu wa City kusaini mkataba mpya tangu wiki iliyopita baada ya Nicolas Otamendi na Fernandinho.

0 comments:
Post a Comment