GWIJI
wa England na mtangazaji mwenye heshima kubwa, Jimmy Armfield amefariki
dunia akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
saratani.
Pamoja
na kuichezea mechi 569 Blackpool enzi zake, Armfield pia alikuwa
Nahodha wa England mara 15 katika mechi 43 alizochezea Simba Watatu.
Baada
ya kuwa kocha wa timu za Leeds na Bolton, Armfield akahamia kwenye
utangazaji na kujivunia heshima kubwa akiwa mchambuzi wa BBC Radio 5
Live.
Familia
yake imethibitisha kifo chake kilichotokea Trinity Hospice mapema
asubuhi ya leo. Mungu ampumzishe kwa amani gwiji huyo. Amin.
Jimmy Armfield akipokea tuzo maalum ya Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) mwezi Aprili mwaka 2008

0 comments:
Post a Comment