Wednesday, January 31, 2018


Usiku wa jana umeendelea kuwa mbaya kwa vijana wa Arsene Wenger, Arsenal wamekubali kipigo cha mabao 3 kwa 1 kutoka kwa Swansea kipigo ambacho kinaonekana kuwakera wana Arsenal wengi, nini nilikiona?
1.Lazima wamnunue Aubameyang, Arsenal wanahitaji “world class striker” usajili wa Aubameyang kwa hali yao ya sasa sio hiari ni lazimana hii haitawasaidia tu katika kufunga mabao bali inaweza kuamdsha hamasa ya wachezaji inayoonekana kulala.
2.Giroud ni mchezaji wa Arsenal. Wengi habari za jana tuliamini huenda Giroud ameshaingiza mguu mmoja Stamford Bridge lakini tofauti na wengi wakivyofikiri mshambuliaji huyo alikuwepo jana katika uwanja wa Liberty Stadium.
3.Cech ameanza kuwa tatizo. Sio tu katika mechi ya jana lakini Cech siku za usoni ameonekana sio Cech yule wa Chelsea na usiku wa jana lawama nyingi alitupiwa yeye akionekana kufungwa mabao ya kirahisi sana.
4.Ayews wanaweza kuwa mhimili wa Swansea. Jana Jordan alionekana tatizo kwa Arsenal kwa jinsi alivyoisumbua beki yao na akafanikiwa kufunga moja ya bao kati ya mabao 3 ya jana na hivi karibuni mdogo wake anataraji kujiunga naye.
5.Swansea wanaanza kujiamini. Kati ya matatizo ambayo yalikuwa yakiisumbua Swansea ni kujiamini, lakini mchezo dhidi ya Arsenal walionekana kucheza vizuri sana mbele ya Arsenal na kidoogo wanaonekana kuanza kurudi katika fomu yao.

0 comments:

Post a Comment