Wednesday, January 31, 2018



Arsenal imekubali kumuuza mshambuliaji wake wa Kifaransa Olivier Giroud kwenda Chelsea kwa pauni milioni 18.

Kuondoka kwa Giroud  kunafuatia ujio wa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang   anayetua Arsenal akitokea Borussia Dortmund kwa usajili unaovunja rekodi ya klabu - pauni milioni 55.5.

Giroud aliichezea Arsenal mechi yake ya mwisho Jumanne usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ulioshuhudia Arsenal ikilala 3-1.

0 comments:

Post a Comment