AlanTarsis-SPORTS
Searching...
Select a Page
  • Home
  • Kitaifa
  • Kimataifa
Home » »Unlabelled » Tetesi za Soka Jumanne 23.01.18
Tuesday, January 23, 2018

Tetesi za Soka Jumanne 23.01.18


Aymeric Laporte
Manchester City inamtaka Aymeric Laporte na inafikiria kutimiza kipengee cha kumruhusu beki wa kati huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 kilichotolewa na Athletic Bilbao cha Pauni milioni 60. (Sun)
Borussia Dortmund inamtaka mshambuliaji raia wa Ufaransa wa timu ya Arsenal Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 31, kama sehemu ya kubadilishana na mchezaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa 28, - au wasitishe mpango huo hadi msimu wa joto. (Mirror)
Chelsea inatafakari kuvunja sera ya kutolipa malipo ya uhamisho kwa wachezaji wake kando na makipa walio na umri wa miaka 30, kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, kutoka Roma. Upande wa Antonio Conte huenda ukakamilisha makubaliano ya mara mbili ya Dzeko na mchezaji wa Roma Italia wa kiungo cha beki kushoto Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 23, kwa thamani ya pauni milioni 44. (Telegraph)
Dzeko apewa kadi nyekundu kwa kumvua mwenzake suruali
Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma
Kane na Kante waorodheshwa kushindania Ballon d'Or
Au Chelsea itawalipia wachezaji wote wawili pauni milioni 50. (Mirror)
Crystal Palace imeanzisha mazungumzo na Inter Milan kuhusu makubaliano ya zaidi ya pauni milioni 8.5 kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele Eder, mwenye umri wa 31. (Mail)
Newcastle ipo tayari kusaini uhamisho wa mkopo wa winga wa Chelsea raia wa Brazil Kenedy, mwenye umri wa miaka 21, katika saa 24 zijazo. (Mail)
Mohamed Salah
Real Madrid inajitayarisha kwa uhamisho wakati wa msimu wa joto wa Mohamed Salah wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 kwa mujibu wa rais wa shirikisho la soka Misri. (Liverpool Echo)
Newcastle inashughulikia makubaliano ya kumleta mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Ufaransa Kevin Gameiro, mwenye umri wa miaka 30, kuingia St James' Park. (Express)
Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 29 yupo nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguuu wake uliovunjika. (Telegraph)
Wasiwasi kuhusu afya ya Fabian Delph unamaanisha kuwa Manchester City inatazamia kumsaini mchezaji wa Shakhtar Donetsk kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 24 Fred hivi sasa, badala ya kusubiri hadi msimu wa joto. (Manchester Evening News)
Winga wa Brazil Lucas Moura, 25, anayelengwa na Tottenham, anasema "hana raha" akiwa Paris St-Germain. (L'Equipe)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe anasema kurudi kwa winga Junior Stanislas, na mshambuliaji wa Norway Joshua King, mwenye umri wa miaka 26, kutoka kuuguza majeraha, ni kama kuwasajili wachezaji wawili. (Bournemouth Echo)
at January 23, 2018
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Next
Newer Post
Previous
Older Post

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

ZILIZOTAZAMWA KWA WINGI

  • MAJENGO PACHA YA SIMBA NA PILIKA ZAKE MTAA WA MSIMBAZI
    Majengo pacha ya klabu ya Simba yaliyopo Mtaa wa Msimbazi mjini Dar es Salaam yanavyoonekana kwa mbele. Jengo la kushoto lipo tangu ...
  • Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 27.08. 2019: Sanchez, Neymar, Vinicius Jr, Bony, Matic, Monreal
    Huenda Manchester United ikasubiri ukaguzi wa mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 23, ...
  • Zifahamu takwimu za Messi, Ronaldo na Van Dijk kabla ya mshindi kujulikana usiku wa leo
    Uefa leo Alhamisi inatarajiwa kumtangaza mchezaji bora wa mwaka wa soka Barani Ulaya . Waliojumuishwa katika orodha ya kushindania tuzo h...

Kuhusu

HABARI MPYA

AlanTarsis-SPORTS

Michezo na Burudani (ULIMWENGU WA MICHEZO)

PERUZI HAPA

  • BASKETBALL
  • FOOTBALL
  • KIMATAIFA
  • RIADHA
  • TENES
 
Copyright © AlanTarsis-SPORTS All Right Reserved
Blogger Designed by: Sharifu Majaindila | Sharifu salehe
Alana • Matambalira