Friday, February 16, 2018


Michy Batshuayi anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund kutoka Chelsea, akishangilia baada ya kufunga mabao mawili dakika za 65 na 90 na ushei wenyeji wakitoka nyuma kwa mabao 2-1 na kushinda 3-2 dhidi ya Atalanta kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Europa League usiku wa Alhamisi Uwanja wa Signal-Iduna-Park mjini Dortmund. Bao lingine la Dortmund lilifungwa na Andre Schurrle dakika ya 30, wakati ya Atalanta yalifungwa na Josip Ilicic yote dakika za 51 na 56

0 comments:

Post a Comment