“Mtoto yake nepi” Real Madrid wamedhihirisha msemo baada ya
usiku wa leo kutoka nyuma kwa bao 1 kwa 0 mbele ya PSG na kisha
kuumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao 3 kwa 1.
Cristiano Ronaldo alikuwa shujaa wa Real Madrid baada ya kuweka
kambani mabao mawili ambapo sasa nakuwa na mabao 116 na ni timu 19 tu
katika Champions League ndio zimefunga mabao mengi zaidi yake.

Liverpool
nao waliangusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Fc Porto baada ya kuwapiga
mkono(mabao 5) huku utatu wa Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto
Firminho ukiendelea kuwa cancer kwa wapinzani.

Sadio
Mane alifunga mabao 3 na kumfanya kuwa mchezaji wa 3 kwa Liverpool
kufunga hattrick chini ya Jurgen Klopp baada ya hattrick za Divick Origi
(Dec 2015) na ile ya Phillipe Coutinho(2007).
0 comments:
Post a Comment