Thursday, February 1, 2018


Hofu mpya imetanda kuelekea michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 ambapo sasa kimekuwa na wasiwasi kwamba ibuko kubwa la wadudu aina ya panzi nchini Urusi inaweza kuathiri viwanja nchini humo.
Kumeibuka homa ya panzi Kusini mwa Urusi na baadhi ya sehemu nchini Urusi ambayo inaathiri mimea na mamlaka inayobusiana na kilimo imeonya kwamba huenda madhara hayo yakahamia katika viwanja.
Panzi hao wamekuwa wakila sana majani na kuharibu kabisa mimea sehemu nyingi katika nchi ya Urusi na sasa wanaweza kuelekea uwanjani kushambulia majani.
Mmoja wa maofisa wanaohusiana na masuala ya kilimo amesema mara kadhaa tatizo la panzi limekuwa likitokea nchini Urusi na wamekuwa wakikabiliana nalo lakini safari hii wana hofu kubwa kwamba huenda suala hilo litaibua skendo kubwa.
Maeneo kama Volgogard ambao ni mji ambao hauko mbali na Moscow hali inatajwa kuwa mbaya na tayari baadhi ya viwanja vidogo vilivyo pembezoni mwa Urusi vimeshaanza kuharibiwa na panzi.
Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuanza mwezi June tarehe 14 mwaka huu hadi July 15 ambapo viwanja 12 katika miji tofauti nchini humo vitatimka vumbi.

0 comments:

Post a Comment