Rais wa Fifa, Gianni Infantino anaongoza kikao cha siku moja kujadili
masuala mbalimbali kuhusu soka la vijana na wanawake na maendeleo ya
mchezo wake kwa jumla.
Mara baada ya kuwasili ukumbi hapo akiwa katika msafara wa magari manne,
Infantino aliyefuatana na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad pamoja na Rais wa
TFF, Wallance Karia, Mjumbe wa CAF na mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga
na Kaimu Katibu wa TFF, Wilfred Kidau alivalishwa mgolole na wamasai
waliokuwa akicheza ngoma nje ya ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Rais huyo wa FIFA baada ya kuvalishwa mgolole pamoja na Rais wa CAF,
alivalishwa bangili na alipewa kirungu kiilichotengenezwa kwa kisu.
Walipoingia ndani ya jingo hilo, walipata zawadi maalumu kutoka Bodi ya
Utalii Tanzania pamoja na nakala zinazozungumzia Tanzania na hifadhi
zake.
Awali wajumbe kutoka nchi 19 walitangulia wakiongozwa na Katibu mkuu wa
Fifa, Fatma Samoura ambaye naye alionekana kufurahia mapambo ya kimasai
kwa wamasai waliokuwa wakiuza bidhaa zao.
Home
»
»Unlabelled
» Rais wa FIFA Apagawa na Nguo za Kimasai Alizovalishwa
Thursday, February 22, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment