
Tottenham wana nia
ya kumpa meneja Mauricio Pochettino mkataba mpya wa pesa nyingi. Raia
huyo wa Argentina aliweka sahihi mkataba mpa ya miaka mitano mwaka 2016
wa pauni milioni 5.5 kwa mwaka. (Telegraph)
Real Madrid wanaongoza
mbio za kumwinda mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld. Manchester
City, Chelsea na Manchester United pia nao wanamwinda mbelgiji huyo wa
miaka 28. (Mirror)
Jeventus wameuliza kuhusu kiungo wa kati wa Liverpool Jack Wilshere ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu. (Mirror)
Everton na Tottenham wote wanamzea mate wing'a wa PSV Steven Bergwijn. Mchezaji huyo wa miaka 20 aliiwakilisha uholanzi katika kwenye kikosi cha chini ya miaka 17 na 21. (ESPN)

Arsenal na Chelsea wote wanafuatilia mkataba wa mlinzi Luke Shaw wa Manchester United. Jose Mourinho amethibitisha kuwa mlinzi huyo yuko katika mkondo wa mkataba mpya lakini mazungumzo bado hayajaanza. (Mirror)

Meneja wa Stoke Paul Lambert anasema kuwa kipa Jack Butland, 24, hataathiriwa na uvumi kuhusu hatma yake (Stoke Sentinel)

Everton wamemsadia shabiki wa miaka 100 kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumualika kwenye mazoezi yao pamoja na kikombe cha chai na mshambuliaji wa zamani wa Everton Duncan Ferguson. (Liverpool Echo)
0 comments:
Post a Comment