Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara msimu huu (2017/18), Simba SC wanaendelea kujifua leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Simba wametwaa ubingwa huo wakiwa na pointi 68 kwenye msimamo wa Ligi huku wakiwa hajapoteza mchezo hata mmoja.
Mechi dhidi ya Kagera Jumamosi ya wiki hii itakuwa ya kukamilisha ratiba itakayoenda sambamba na kukabidhiwa Kombe la Ligi na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakayekuwa mgeni rasmi katika mtanange huo.
Simba watakuwa wanaingia kucheza mechi hiyo bila presha kutokana na ubingwa kuwa mikononi mwao kwa maana hiyo hawana cha kupoteza.
Aidha Simba walichodhamiria ni kumaliza ligi bila kufungwa hivyo wanaenda kupambana na Kagera wakiwa na adham hiyo ili kutengeneza rekodi mpya.
0 comments:
Post a Comment