Timu ya Ruvu Shooting imefanikiwa kuichapa Stand United kwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Mabatini jioni ya leo.
Bao pekee katika mechi hiyo limetiwa kimiani na Rajab Zahir katika dakika ya 73 na kuipa Ruvu pointi tatu muhimu.
Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting iendelee kusalia kwenye nafasi ya 7 ya msimamo wa ligi ikifikisha alama 36.
Wakati huo Stand United imeendelea kubaki kwenye nafasi yake ya 9 ikiwa na pointi 32.
0 comments:
Post a Comment