Friday, May 11, 2018




Kikosi cha Yanga, jana kilikuwa na kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Katika mchezo huo, Yanga imekubali kichapo cha mabao 2-0 0 kutoka kwa wenyeji Prisons, matokeo ambayo yameipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18.

Hali ya kushangaza iliyojitokeza kwenye kikosi hicho cha Yanga ni idadi ya wachezaji waliosafiri na timu kuwa 13 pekee huku benchi la ufundi likiwa na mtu mmoja.

Wachezaji waliosafiri na kikosi ni 

1. Beno Kakolanya
2. Juma Abdul
3. Emmanuel Martin
4. Abdallah Shaibu
5. Pato Ngonyani
6. Maka Edward
7. Paul Godfrey
8. Thaban Kamusoko
9. Yohana Mkomola
10. Matheo Anthony
11. Baruan Akilimali
12. Yusuph Suleiman na
13. Amis Tambwe
Wakati huo benchi la ufundi la Yanga lilionekana kuwa na mtu mmoja pekee ambaye alikuwa ni Kocha Msaidizi wa kikosi hicho, Shadrack Nsajigwa 'Fuso'.
Yanga imefanya tukio hilo likiweka rekodi ya aina yake tangu msimu huu wa ligi kuanza kwa kupeleka idadi hiyo chache ya wachezaji ambao wengi walikuwa ni wa kikosi cha pili.

0 comments:

Post a Comment