Saturday, July 21, 2018

Kocha mpya wa Simba Patrick Aussems amesema falsafa yake katika timu zote alizofundisha ni kumiliki mpira na kutawala mchezo.
Anapenda kuona timu yake ikicheza soka la kuvutia kwa kupiga pasi. Mashabiki wanaolipa viingilio na kukaa jukwaani kuangalia mechi wafurahi na waondoke uwanjani wakiwa wameridhika. Hataki timu inayocheza soka la ‘butua-butua’.
“Falsafa yangu katika vilabu au timu za taifa nilizofundisha ni kuhakikisha tunatawala mchezo, maana yeke timu yangu inatakiwa kumiliki mpira ndio kitu muhimu kwangu”-Patrick Aussems.
“Nahitaji timu yenye mipango, tukiwa hatuna mpira kila mchezaji anatakiwa kujua nini cha kufanya, tukishapata mpira wachezaji lazima wajue wapi mpira unatakiwa kupelekwa.”
“Tunatakiwa kucheza mpira sio kubutua, huo ndio mpango wangu na wachezaji watatakiwa kufuata ili kuwapa burudani mashabiki.”
“Nahitaji kuona mashabiki wakifurahi baada ya kutoka uwanjani kutokana na timu yao kucheza vizuri na kutengeneza nafasi.”
“Sitaki kuona timu inapiga pasi mbili halafu inabutua mpira na hiyo sio falsafa yangu. Wachezaji wanatakiwa kubadilika kutoka walivyokuwa wanacheza misimu iliyopita. Lakini sipo hapa kukosoa makocha wengine waliopita kwa sababu kila kocha alikuja na falsafa yake na mimi falsafa yangu ni timu kucheza soka la kuvutia na ushindani ambalo litaridhisha mashabiki wanaokuja uwanjani.”
“Bado sijakutana na wachezaji, jambo la kwanza kuwaeleza itakuwa ni falsafa yangu. Nataka kuona kila mchezaji anafurahi wakati anacheza uwanjani.”

0 comments:

Post a Comment