KIUNGO
Philippe Coutinho amepewa jezi namba saba (7) Barcelona kutoka namba 14
aliyokuwa anavaa tangu amejiunga na timu hiyo Januari mwaka huu
akitokea Liverpool.
Jezi hiyo ambayo imewahi kuvaliwa na magwiji kama Luis Figo, David Villa na Henrik Larsson, awali ilikuwa inavaliwa na Arda Turan, ambaye ametolewa kwa mkopo Istanbul Basaksehir na kuiacha wazi.
Mara ya mwisho Coutinho kuvaa jezi namba 7 ilikuwa katika msimu wake wa mwisho Inter Milan kabla ya kujiunga na Liverpool mwaka 2013. Alipokuwa Liverpool, alikuwa anavaa namba 10.
Philippe Coutinho amepewa jezi namba saba (7) Barcelona kutoka namba 14 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barcelona Januari kwa dau la Pauni Milioni 145, na mara moja kugeuka kuwa mchezaji muhimu Nou Camp, akifunga mabao 10 katika mechi 22 katika nusu ya pili ya msimu uliopita.
Pia aling'ara katika Kombe la Dunia akifunga mabao mawili kabla ya Brazil kutolewa katika Robo Fainali na Ubeligiji.
Mchezaji aliyedumu kwa muda mrefu na jezi namba 7 ya Barcelona ni Charly Rexach, winga aliyecheza mechi zaidi ya 300 miaka ya 60 hadi 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80.
Lakini mfumo wa namba za jezi ulitambulishwa rasmi Barcelona kuanzia msimu wa 1995/96, wakati timu ikiundwa na wakali kama Eidur Gudjohnsen na Pedro.
Si kila aliyevaa jezi namba 7 Barca alifanikiwa, kwani hata mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Alfonso Perez alipewa jezi hiyo baada ya kujiunga na timu mwaka 2000, wakati mshambuliaji Muargentina, Javier Saviola alishindwa kung'ara.

0 comments:
Post a Comment