Ronaldo goli lake alilolifunga dhidi ya Juventus msimu uliopita akiichezea Real Madrid ndio goli bora la UEFA na baada ya kushinda tuzo hiyo Ronaldo aliizungumzia ishu ya kufunga goli hilo.
“Niliona mpira ukiwa juu na nikasema ngoja nijaribu labda inawezekana nitashindwa kuugusa lakini najaribu, nilifanikiwa kuugusa na namna nilivyougusa ulienda moja kwa moja kwa nguvu katika goli, nilivyoanguka chini naangalia mpira huko nyavuni”
“Nikasema waooh!! nimefanikisha nilishikwa na mshangao lakini wakati huo huo sikushangazwa sana kwa sababu kwa muda mrefu nimekuwa nikijaribu kufunga goli katika robo fainali lakini kufunga katika game za kufuzu ni fahari sana”
0 comments:
Post a Comment