MAMBO yamekwenda ndivyo sivyo kwa straika wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye
alionekana anaweza kuwa fiti kucheza leo lakini hali yake imebadilika
na hatacheza dhidi ya Mbeya City leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar.
Okwi aliumia hivi karibuni katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Alionekana kuweza kuiwahi Mbeya City lakini juzi Jumamosi uongozi wa
benchi la ufundi la Simba unaoongozwa na Mbelgiji, Patrick Aussems,
ulilazimika kumpatia muda wa mapumziko mshambuliaji huyo kutokana na
kushindwa kufanya mazoezi.
Uongozi huo ulifikia hatua hiyo baada ya Okwi kudai kuwa anahisi maumivu
makali ya kiuno, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya mazoezi kama
ilivyo kawaida yake.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatatu
limezipata zimedai kuwa hali hiyo ililimfanya Aussems pamoja na daktari
wa timu hiyo, Yassin Gembe kumpeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa
vipimo lakini pia akataka Okwi kuwa nje ya uwanja mpaka hapo atakapokuwa
amekaa sawa.
“Jana (juzi) alifanyiwa vipimo kwa dokta mmoja hivi ambaye ni mtaalamu
wa viungo na majibu yake yatatoka leo (jana) ili kujua ni nini
kinachomsumbua zaidi ili aweze kupata matibabu.
“Lakini pia kama vipimo havitaonyesha tatizo lolote basi atatakiwa
kupmzika kwa muda ili aweze kuwa sawa, kwa hiyo kuanza sasa hatafanya
mazoezi tena mpaka hapo kocha atakapojiridhisha kuwa hana tena maumivu
na yupo sawa,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipotafutwa Okwi ili aweze kuzungumzia hilo, hakupatikana kama
ilivyokuwa kwa dokta wa timu hiyo Yassin Gembe lakini meneja wa timu
hiyo, Richard Robert alijibu kwa kifupi: “Bado hajakaa sawa ila
maendeleo yake siyo mabaya na anaendelea kupata matibabu.”
Home
»
»Unlabelled
» Okwi Mambo Yamuendea Hovyo Leo Kuikosa Mechi Yao Dhidi ya Mbeya City
Monday, August 27, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment