Luka Modric amemua
kubaki Real Madrid. Kiungo huyo wa kati raia wa Croatia mwenye miaka 29
amehusishwa na kuhama kwenda Inter Milan. (AS - in Spanish)
Modric atasaini mkataba mpya na kupandisha mshara wake kufikia ule wa nahodha Sergio Ramos. (Marca)Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba anataka kubaki kwenye klabu (RMC Sport - in French)
Wolves wamijiwekea lengo la kishinda Ligi ya Premio katika kipindi cha miaka saba. (Times - subscription required)
Beki mpya wa Fulham mwenye miaka 24 Joe Bryan alibadili mawazo yake kuhusu kuelekea Aston Villa akiwa safarini na kikosi hicho wakati wa mazoezi baada ya kupita uchunguzi wa kiafya. (Bristol Post)
Kiungo wa kati wa Aston Villa mwenye miaka 22 Jack Grealish atapewa mkataba mpya na pauni milioni 30 za kununua mkataba wake. (Sun)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City Stephen Ireland, 31, anafikiria kuhama Ujerumani baada ya kundoka Stoke City mwisho wa msimu. (Mail)
Kiungo wa kati wa Croatia mwenye miaka 20 Nikola Vlasic anaratajiwa kujiunga na CSKA Moscow kwa mkopo (Sport24 - in Russian)
Meneja ya Everton Marco Silva amemuambia mshambuliaji Ademola Lookman, 20, abaki klabuni na apiganie nafasi yake. (Telegraph)
Paris St-Germain walikataa ofa ya Manchester United kwa mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 19. (Mirror)
PSG wanataka kumsaini wing'a wa Barcelona Ousmane Dembele na kumuunganisha na meneja homas Tuchel aliyemsiamia mchezaji huyo wa miaka 21 huko Borussia Dortmund. (Mail)
Bora zaidi kutoka Ijumaa
Meneja wa United Mourinho anaamini wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amekuwa akiidhuru klabu hiyo kwa kujaribu kumuuza Mfaransa huyo mwenye miaka 25 kwa Barcelona na Juventus. (Times)
United waliikataa fursa ya kumchukua beki wa kati wa Leicester na England Harry Maguire, 25, kwa £15m mwaka jana. Lakini mwaka huu wamekuwa wakimtafuta sana na hawakufanikiwa kumnunua (Telegraph)
Everton watalazimika kusubiri hadi Ijumaa asubuhi kubaini iwapo ombi lao la kumtaka beki wa Ufaransa mwenye miaka 23 Kurt Zouma kutoka Chelsea kwa mkopo limekubaliwa. (Liverpool Echo)
Beki wa kushoto wa Tottenham mwenye miaka Danny Rose bado anataka sana kuhamia Paris St-Germain kwa mkopo. (Sun)

0 comments:
Post a Comment