Friday, September 7, 2018



Bingwa wa soka kutoka Argentina Diego Maradona ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya daraja la pili nchini Mexico Dorados de Sinaloa.

Mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 57 aliwahi kucheza mara 91 kwa nchi yake kati ya 1977 na 1994 na pia ameifunza timu hiyo ya taifa tangu 2008 hadi 2010.

Mara ya mwisho kukifunza klabu ilikuwa ni Al-Fujairah katika Umoja wa falme za kiarabu mkataba uliomalizika April.

Kwa mujibu wa BBC, Vyombo vya habari Mexico vinadai Maradona ameajiriwa kuichukuwa nafasi ya Francisco Gamez, aliyefutwa kazi kama kocha mnamo Alhamisi.

Katika kanda fupi ya video kwenye mtandao wa kijamii, klabu hiyo iliweka ujumbe wa kumkaribisha Maradona uliosema 'Karibu Diego', na 'Timiza 10', nambari iliyokuwa kwenye jezi ya Maradona alipokuwa mchezaji.

Maradona alizichezea timu za Argentinos Juniors, Boca Juniors, Barcelona na Napoli miongoni mwa timu nyingine alipokuwa akicheza soka ya kulipwa na atazamwa na wengi kama mojawapo ya wachezaji bora wa soka.
07 Sep 2018

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.