Kiungo mshambuliaji wa Uholanzi, Wesley Sneijder, ametangaza rasmi jana kustaafu mchezo wa soka la kimtaifa.
Sneijder alifikia maamuzi hayo kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika dhidi ya Peru.
Akiwa na timu ya taifa, Sneijder ameichezea kwa miaka 15 na kufanikiwa kucheza mechi 134 huk akifunga mabao 31 na nafasi za kutengeneza 31.
Kiungo huyo ameisadia Uholanzi kufika nusu fainali ya Michuano ya Euro 2004, robo fainali mwaka 2008, kufika fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 na kuwa washindi wa tatu kombe la dunia 2014 huko Brazil.
0 comments:
Post a Comment