Mshambuliaji mwenye kasi ya hatari ndani ya kikosi cha Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa, amesema anaamimi bado ana uwezi wa kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars, imeelezwa.
Ngasa ambaye msimu uliopita alikuwa na Ndanda FC na sasa Yanga anaamini ataweza kuonesha makali yake endapo akipewa nafasi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Ngassa amesema hajawahi kutangaza kustaafu Stars hivyo bado ana imani ana uwezi wa kumrejesha na kuichezea timu hiyo.
Ngassa amesema anatamani na anaamini anaweza kurejea katika nafasi yake ya awali kutokana na namna anavyojifua hivi sasa akiwa na Yanga.
Wakati Ngasa akifunguka hayo, Stars ilikwenda suluhu ya 0-0 na Uganda The Cranes kwenye Uwanja wa Nelson Mandela huko Kampala jana kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019.
0 comments:
Post a Comment