Pamoja
na wengi kumuangalia zaidi Jose Mourinho wa Manchester United, Kocha wa
Madrid, Julen Lopetegui anaonekana ndiye kocha mwenye hofu zaidi ya
kupoteza kibarua chake, miezi 3 tu baada ya kuanza kazi.
Tayari kapoteza mechi ya ligi, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Super Cup na harufu ya kufutwa kazi, tayari inanunikia.
Wakati
anatua Madrid, mwanzoni kabisa ya michuano ya Kombe la Dunia, Lopetegui
alionekana kuwa na wakati mgumu baada ya kuondoka kwa Kocha Zinedine
Zidane.
Hata
kama kocha huyo aliondoka, lakini kocha huyo raia wa Hispania alijiunga
na Madrid baada ya nyota wake, Cristiano Ronaldo naye kuwa ameondoka na
kujiunga na Juventus ya Italia.
Hii imemfanya kocha huyo kuzidi kuwa na wakati mgumu na sasa analazimika kutengeneza kila kitu upya.
Lakini
ubaya wa Madrid ni kutochelewesha kocha anayeyumba na hii inamfanya
kuwa kocha mwenye hofu zaidi na kazi yake kwa kipindi hiki.
0 comments:
Post a Comment