Uongozi
wa Singida United na klabu ya Mamelod Sundowns uko kwenye hatua za
mwisho kuweza kufikia makubaliano ya kumuuza nyota wa Singida United
Habibu Kyombo, aliyefanikiwa kufuzu majaribio kwenye klabu hiyo.
Kyombo
alikwenda kufanya majaribio katika klabu ya Mamelod mapema Agosti 20,
mwaka huu, kwa muda wa siku kumi na baadaye waliweza kumuongezea siku
nyingine zaidi kuweza kumuangalia na sasa inaelezwa kuwa ameshafuzu.
Taarifa
za ndani kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa tayari mambo yanaenda
vizuri kwa klabu hizo mbili na wakati wowote Kyombo anaweza kuondoka na
kujiunga na klabu yake hiyo mpya.
“Kyombo
mambo yake tunaweza kusema kwa upande mwingine yapo hatua za mwisho
kabisa, ni asilimia 90, bado 10 tu. Sababu timu zimeshakubaliana kwa
asilimia kubwa kilichobaki ni kidogo na dili likikamilika tu anaweza
kuondoka muda wowote na kujiunga na klabu yake mpya ya Mamelod ambapo
alifanikiwa kufuzu majaribio,” kilisema chanzo.
0 comments:
Post a Comment