BAADA
ya kuzuka ghafla kwa taarifa kuwa ndani ya uongozi wa Klabu ya Simba
hakuna maelewano huku ikidaiwa mwekezaji klabuni hapo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwa mbioni kung’atuka, Crescentius Magori amefunguka kila kitu.
Taarifa za Mo kutaka
kuondoka Simba zilianza kusambaa mitandaoni kuanzia Alhamisi lakini
hakukuwa na kiongozi yeyote wa timu hiyo aliyeitisha mkutano wa
wanahabari kwa ajili ya kuweka wazi nini kinaendelea.
Kitendo cha Mo Dewji kuandika
‘caption’ za mafumbo kwenye mitandao yake ya kijamii, kilizidi
kuwavuruga wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imetwaa ubingwa
wa ligi kuu mara mbili mfululizo.
Championi Jumamosi, lilifanikiwa kuzungumza na Magori ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kuhusiana
na ishu hiyo ambapo alisema, kwa sasa hakuna tatizo lolote ndani ya
timu hiyo na kwamba kila kitu kinakwenda sawa kama walivyopanga.
“Hakuna mgogoro wowote ndani ya Simba,
kwa sasa kila kitu kinakwenda kama ambavyo kimepangwa, mashabiki wa
Simba wanapaswa watulie wasifuate taarifa ambazo hazina ukweli,”
alisema Magori.
Naye Mwenyekiti wa Simba, Suedy Mkwabi alisema: “Kwa sasa nipo nchini China,
nashughulikia masuala ya biashara zangu, hivyo masuala ya migogoro
ndani ya Simba mimi sifahamu, najua kwamba kila kitu kipo sawa.”
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mo Dewji, jana aliandika kwamba: “Kwenye
uongozi na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na
sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi
mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao.”
0 comments:
Post a Comment