Friday, July 5, 2019

Golikipa wa Singida United asajiliwa na Gor Mahia ya Kenya


Golikipa wa Singida United, David Kissu amesaini kandarasi ya miaka mitatu ya kuitumikia klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kijana wao Kissu kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwenye klabu kubwa Nchini Kenya na Africa Mashariki.

"Tunashukuru mchezaji wetu kupata nafasi hii ya kwenda kucheza Gor Mahia na huu ni mwendelezo wa klabu yetu kuwaruhusu na kuwatafutia nafasi wachezaji wetu kucheza kwenye klabu kubwa kuliko sisi ndani na nje ya nchi" Sanga

0 comments:

Post a Comment