SADIO Mane, mshambuliaji wa Liverpool amewafungia vioo Real Madrid ambao walikuwa wanahitaji saini yake msimu ujao.
Mane inasemekana kuwa yupo kwenye hesabu za Kocha wa Madrid, Zinedine Zidane ambaye anahitaji kuboresha kikosi chake.
Klabu hiyo ilikuwa inampigia hesabu Mane, ghafla ilisitisha mpango huo na kuongeza nguvu Kwa Neymar Jr ambaye naye alizingua na amebaki PSG bila kupenda.
Zidane inaelezwa kuwa kwa udi na uvumba anaisaka saini ya nyota huyo anayekipiga Timu ya Taifa ya Senegal.
Kibabe, Mane amesema kuwa timu zisijisumbue kuisaka saini yake Kwa sasa. "Sifikikirii kusepa ndani ya Liverpool kwa sasa, tumefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa nataka kuisaidia timu kutwaa Ligi Kuu England," amesema.
Mara ya mwisho, Liverpool kutwaa ubingwa wa England ilikuwa msimu wa mwaka 1989/90.
0 comments:
Post a Comment