
Kiungo wa kati wa
Arsenal Mesut Ozil, 31, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki ya
Fenerbahce kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha la uhamisho la mwezi
Januari. (Fotomac, via Football.London)
Manchester United
haitaruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kuondoka kuelekea
Real Madrid katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)Wachezaji wa United na maafisa wameshawishika kwamba Pogba ameichezea klabu hiyo mechi yake ya mwisho na atandoka mwezi Januari. (Mirror)
Iwapo Carlo Ancelotti atakuwa mkufunzi mpya wa
Everton uhamisho wake wa kwanza utakuwa jaribio la kumsaini mshambulaji
wa zamani wa Man United Zlatan Ibrahimovic, 38. Raia huyo wa Sweden atakuwa mchezaji aliye huru wakati kandarasi yake na LA Galaxy itakapokamilika. (Calcio Mercato)
Aliekuwa beki wa Everton Alan Stubbs ametuma pongezi kwa Duncan Ferguson na jinsi alivyoisaidia Everton kama kaimu meneja , akisema kwamba uteuzi wa Ancelotti hautawezekana bila kuwepo kwa mchezaji huyo wa zamani. (Talksport)
Chelsea ni miongoni mwa klabu za ligi ya Premia zinazotarajia kumsaini winga wa Real Madrid na Brazil Vinicius Junior, 19, mnamo mwezi Januari.

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anaongoza baadhi ya wachezaji wa klabu ya Arsenal ambao wanafikiria kuhusu hatma yao katika klabu hiyo. (Independent)
Klabu ya Bruges nchini Ubelgiji inataka Yuro milioni 30 ili kumuuza mshambuliiaji wake Emmanuel Dennis huku klabu za Leicester, Brighton ana Southampton zikiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia. (Foot Mercato, via Leicester Mercury)

Manchester United italazimika kulipa dau la £12m kwa ajenti Mino Raiola juu ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa RB Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19. (Sun)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Brazil Lucas Moura, 27, amekiri kwamba alikaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2012 kabla ya kuamua kujunga na PSG badala yake. (ESPN Brasil, via Mirror)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 25, anaweza kutoa ombi la kutaka kuhamia Juventus akiendelea kutafuta nafasi ya kwanza katika klabu hiyo.. (Goal)
Tetesi bora za Alhamisi
Manchester City wanataka walipwe pauni milioni moja
ili wavunje mkataba na kocha wao msaidizi Mikel Arteta - Arsenal
wanataka kumtangaza Arteta kama kocha wao mkuu mpya. (Mail)Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 23, baada ya kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japani na klabu ya Red Bull Salzburgforward Takumi Minamino, 24. (Star)

Carlo Ancelotti anatarajiwa kutangazwa kama kocha mpya wa Everton baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 11.5 kwa mwaka. (Mirror)


0 comments:
Post a Comment