Friday, December 20, 2019



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo limetembelea viwanja vya mazoezi vya Simba vilivyopo Bunju, nje kidogo ya Dar es Salaam na kutoa neno la pongezi kwa Simba kwa hatua ambayo wamefikia.

Viwanja hivyo vya Simba vimepewa jina la Mo Simba Arena kimoja ni cha nyasi bandia na kingine ni cha nyasi asilia maalumu kwa ajili ya mazoezi.

Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya TFF, Oscar Mirambo amesema kuwa“Niwapongeze Simba kwa hatua ambayo wamepiga kwa kuwa na viwanja ambavyo tumekuwa na uhaba navyo. Hii inamaana kwamba kama nchi sasa tunapiga hatua,",

0 comments:

Post a Comment