Wednesday, February 19, 2020



Matembo wa soka la Uhispania, klabu ya soka ya Real Madrid imemwagisha wino na kumuongeza kwenye kikosi chake nyota (18), kiungo kutokea Brazil,  Reinier Jesus Carvalho.

Akizungumza wakati wa utambulisho katika dimba la Santiago Bernabeu, nyota huyo aliyepata uhamisho kutokea klabu ya soka ya Flamengo ya Brazil alisema anataka kuwa sehemu ya historia ya mafanikio ya klabu hiyo.

“Nijuavyo mimi hakuna aiseifahamu Real Madrid, nimefurahi sana, hizi ni siku bora zaidi za maisha yangu, Real Madridi ni timu kubwa na siku zote imekuwa ni timu ya ndoto yangu. Nitajitolea kwa uwezo wangu wote kwa ajili ya timu hii. Ndoto zangu za utotoni zimegeuka kuwa kweli. Nataka kuwa sehemu ya historia ya timu hii”.

Kwa hivi sasa nyota huyo atakuwa akiichezea timu B ya Real Madrid inayocheza ligi ya daraja la tatu, na atashuka dimbani katika mechi ya timu hiyo na Castilla. Mchezaji huyo atajiunga katika mazoezi ya timu A kulingana na matakwa ya kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane.

Vyombo vya habari nchini Uhistpania vinadai kwamba Real Madrid imelipa Euro milioni 30 kwa ajili ya uhamisho wa nyota huyo.

0 comments:

Post a Comment