
Kiungo wa kati wa
Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu
lakini klabu hiyo inataka zaidi ya £150m kumuachilia mchezaji huyo wa
miaka 26. (ESPN)
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola anasema kuwa ana
mpango wa "kuwasiliana" na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar
Solskjaer baada ya majibizano makali kumhusu mteja wake. (Sky Sports)Ndugu wa Pogba wa kiume Mathias anasema kuwa "kila mtu anajua" kwamba anataka kuondoka Manchester United "kwenda kucheza soka ya Champions League na kushinda mataji". (Sun)
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ataelekezewa darubini kali ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Champions League msimu huu. (Telegraph)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kuwasajili mkurugenzi wa zamani wa michezo Paris St-Germain Antero Henrique na mkuu wa michezo wa Red Bull Ralf Rangnick katiki wadhifa wa mkurugenzi wa kiufundi. (Independent)
Beki wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 21, amesema anajua kuwa ''ananyatiwa'' na Barcelona na Arsenal. (RMC Sport, via Goal)

Barcelona inamlenga mshambuliaji wa Denmark na Leganes Martin Braithwaite, 28, baada ya kupewa ishara ya kumtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, baada ya kusitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad Mrazil Willian Jose, 28. (Sky Sports)
0 comments:
Post a Comment