
Mlinda
mlango wa Simba, Aishi Manula hajakaa langoni kwenye klabu hiyo tangu
alipodaka katika mchezo wa ligi wa Simba dhidi ya Yanga, Januari 4,
2020.
Katika
mchezo huo, Manula alilalamikiwa na mashabiki wa Simba hasa katika bao
la pili alilofungwa na kupelekea mchezo kuisha kwa sare ya maba0 2-2,
huku Yanga wakiibuka mashujaa kwa kutoka nyuma kufungwa mabao hadi
mchezo kumalizika kwa sare.
Tangu
mchezo huo, imepita jumla ya michezo tisa, Aishi Manula hajaanza golini
na nafasi yake ikichukuliwa na mlango Beno Kakolanya.
Baada
ya mchezo wa Simba na Yanga, timu ilielekea visiwani Zanzibar kwenye
Kombe la Mapinduzi ambako ilicheza mechi tatu na Beno Kakolanya alicheza
katika michezo miwili huku Aishi Manula akiwa hajakaa langoni katika
mchezo wowote.
Michuano
ya Mapinduzi ilipomalizika na Simba kufungwa katika fainali na Mtibwa
Sugar, timu ilirejea bara kuendelea na ratiba ya ligi na Kombe la
Shirikisho, ambapo katika mechi sita mfululizo mpaka sasa Simba
haijamuanzisha Manula katika mechi zote na badala yake Beno Kakolanya
akianza katika michezo mitano ya ligi na mchezo mmoja wa Kombe la
Shirikisho.
Ni
wazi hilo ni suala linalomuumiza Manula kwani inahatarisha nafasi yake
katika kikosi cha Simba pamoja na timu ya taifa, ikizingatiwa kuwa yeye
ndiye golikipa namba moja wa Taifa Stars kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment