
*********************
Bodi ya ligi ya shirikisho la soka
nchini Tanzania imetangaza mwamuzi Martin Saanya kutoka Mkoani Morogoro
kuwa ndiye mwamuzi atakayepuliza kipyenga katinga mchezo wa watani
wanjadi Kati ya wenyeji Yanga Dhidi ya Simba jumapili ya March 08-2020
uwanja wa Taifa jijini Daresalaam.
Katika mchezo huo Saanya atasaidia
wa mwamuzi Namba Moja (Line One) Mohamed Mkono Kutoka Tanga, Mwamuzi
Namba Mbili (Line Two) Frank Komba wa Daresalaam, Na Mwamuzi wa Mezani
(Fourth Official) Elly Sasii wa Daresalaam.
Lakini katika kile kinachoonekana
Ni kupunguza Malalamiko juu ya waamuzi na kuhakikisha mchezo huo
unachezeshwa kwa ubora TPLB imetangaza waamuzi wawili wa ziada ambao
watasimama kwenye mstari wa goli kwa lugha ya kimpira wanatambuliwa Kama
Goal Line Refferees ambao Ni Abdallah Mwinyimkuu wa Singida Na
Ramadhani Kayoko wa Daresalaam.
Mtathimini was waamuzi katika mechi hiyo atakuwa Ni Sudi Abdi wa Arusha na Kamishina wa mchezo Ni Mohamed Mkweche wa Daresalaam.
Mara ya kwanza na ya mwisho
Tanzania Kutumia muundo huu was waamuzi ilikuwa Ni mwaka 2019 wakati wa
mechi za hatua ya robo Fainali ya Michuano ya Afcon U17 iliyofanyika
jijini Daresalaam.
Mchezo huu wa jumapili unatarajiwa
kuhudhuliwa na Rais wa CAF Ahmad Ahmad ambaye pia atakuwa Ni mgeni wa
Heshima siku hiyo ya mechi
0 comments:
Post a Comment