UONGOZI
wa Azam FC umesema kuwa tatizo kubwa linaloimaliza timu kwa sasa ni
ubutu wa safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa mwenye
mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, amesema kuwa
wamekuwa wakiutazama mwenendo wa timu na aina ya matokeo jambo
linalowafanya watafute mbinu ya kulimaliza tatizo hilo pale ligi
itakapomalizika.
“Kweli
tuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji hilo lipowazi lakini kwa sasa
hatuwezi kufanya jambo lolote kulimaliza tulichokubaliana ni kwamba
tuboreshe mikataba kwanza ya wachezaji tulionao kisha kwenye dirisha la
usajili tutaleta washambuliaji ambao watakuwa suluhisho la tatizo letu,”
amesema.
Ligi
Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kupisha maambukizi
ya Virusi vya Corona, safu ya Azam FC imefunga mabao 37 na safu ya
mabeki imeruhusu mabao 20 kwenye mechi 28.
0 comments:
Post a Comment