NAHODHA
na beki wa kati wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto amekiri kuwepo
kwenye mazungumzo mazuri ya kukamilisha dili lake la kusaini mkataba wa
miaka miwili ya kukipiga Yanga.
Beki huyo ni kati ya
wachezaji waliokuwepo kwenye mazungumzo ya kukamilisha usajili wake wa
kutua Yanga katika kuboresha safu ya ulinzi ya timu hiyo inayochezwa
hivi sasa na Mghana, Lamine Moro, Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’
na Juma Makapu.Staa huyo wa Coastal hivi karibuni alikuwa anatajwa
kwenye usajili wa Simba kuelekea msimu ujao kabla ya Yanga chini ya
wadhamini wao GSM kuingilia kati dili hilo la usajili.
Akizungumza
na Championi Ijumaa, Mwamnyeto alisema kuwa Yanga wapo kwenye hatua za
mwisho na mabosi wa klabu hiyo kukamilisha usajili wake wa kutua
Jangwani.
Mwamnyeto
amekiri kufuatwa na baadhi ya klabu za ndani na nje ya nchi
zilizomfuata ambazo wameshindwana katika maslahi huku akiitaja Yanga
ndiyo iliyokuwepo katika hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo la
usajili.
Aliongeza
kuwa kikubwa kilichompeleka Yanga ni maslahi mazuri na siyo kitu kingine
ambapo yeye mwenyewe amekubaliana na hivi karibuni atasaini mkataba wa
awali.
“Nipo kwenye
mazungumzo mazuri na Yanga, kikubwa ninachokiangalia hivi sasa ni
maslahi pekee yatakayonifanya nisaini mkataba wa kuichezea Yanga katika
msimu ujao.
“Zilikuwepo
klabu nyingi zilizokuwa kwenye mipango ya kuwania saini yangu lakini
nimeshindwana nazo katika maslahi na siyo kingine, lakini Yanga yenyewe
imeonyesha nia nzuri ya mimi kujiunga nayo.
“Ninafahamu
Yanga upo ushindani mkubwa wa namba, lakini hiyo hainifanyi niogope
kujiunga na Yanga, nimejiandaa kwa ajili ya kupambana na siku zote mimi
siogopi ushindani,” alisema Mwamnyeto.
0 comments:
Post a Comment