![]() |
| Add caption |
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United iko tayari kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 25, anayesemekana kuwa thamani yake ni pauni milioni 70 ya mkataba wa muda mrefu wa pauni 150,000 kwa wiki ili kumsajili mchezaji huyo kutoka Atletico Madrid msimu huu. (Star)
Wakati huohuo, Manchester United inafikiria makubaliano ya mabadilishano ambapo kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, atarejea Juventus huku mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 26, akihamia kwao. (Tuttosport - in Italian)
Matumaini ya Chelsea kumsajili mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak, 27, yameimarika huku klabu ya La Liga ikisemekana kuwa makini kutafuta mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia. (Football London)

Chanzo cha picha, EPA
Kocha wa Barcelona Quique Setien alichaguliwa Januari tu mwaka huu
Kocha wa Barcelona Quique Setien huenda akapigwa kalama baada ya kuchabangwa mabao 8-2 katika Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich Ijumaa - na Mauricio Pochettino, Xavi na Ronald Koeman ndio walio kifua mbele katika orodha ya atakayemrithi Setien huko Nou Camp. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Taarifa za Uhispania zinadai kwamba aliyekuwa kocha wa Tottenham na Southampton Pochettino tayari alishafanya mazungumzo na Barcelona siku nyingi tu kabla ya timu hiyo kuvuliwa nguo Ijumaa. (Express)
Blues huenda ikamtoa mlinga lango wao Kepa Arrizabalaga kwa Atletico kama sehemu ya mabadilishano kwasababu haiko tayari kutimiza bei ya klabu hiyo ya Uhispania ya pauni milioni 110 ili kuwa na mchezaji Oblak. (Star)
![]() |
| Add caption |
Chanzo cha picha, Reuters
Manchester City inajitayarishia kitita cha pauni milioni 40 kumsaka kiungo wa kati wa England na Tottenham Harry Winks, 24. (Sun)
Arsenal iko tayari kuimarisha juhudi zake za kumsajili kiungo wa kati Thomas Partey, 27, kutoka Atletico Madrid. (Star)
Hata hivyo, Gunners huenda ikapata upinzani kutoka kwa Juventus inapowania kumsajili mchezaji huyo wa Ghana. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatua ya Odion Ighalo kuelekea United haikutarajia na wengi
Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo, 31, hana nia ya kujiunga na Paris St-Germain licha ya taarifa kwamba klabu hiyo ya Ufaransa ina nia ya kumsajili raia huyo wa Nigeria, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua hadi Januari. (Manchester Evening News)
Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo anataka Juventus kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Mexico Raul Jimenez, 29, kutoka Wolves kuwa mlengwa wao mkuu msimu ujao. (Gazzetta dello Sport, via Express)
Lille imekataa ofa ya euro milioni 20 euro kutoka kwa Everton kwa ajili ya mlinzi Gabriel, 22, kwasababu wana makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo kwa Napoli, licha ya Arsenal na Manchester United pia kuonesha nia ya kutaka kumsajili raia huyo wa Brazil. (Gianluca di Marzio)

Chanzo cha picha, EPA
Chris Smalling (kushoto) na Cristiano Ronaldo (kulia)
Newcastle inanyatia kumsajili mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye msimu uliopita alikuwa Roma kwa mkopo na pia analengwa na iliyokuwa klabu yake Fulham. (Newcastle Chronicle)
Mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez anasema vilabu 10 Ulaya vimeonesha nia ya kumsajili baada ya mchezaji huyo, 27, raia wa Argentine kuonesha mchezo wa kuridhisha kuelekea mwisho wa msimu. (Marca - in Spanish).
West Brom na West zina zina nia ya kumsajili beki wa Brazil Junior Caicara, 31, kutoka ligi ya mabigwa ya Uturuki, Istanbul Basaksehir. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi
Inter Milan inaweza kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kutoka Barcelona, kulingana na aliyekuwa rais wa klabu ya Serie A club Massimo Moratti. (Quotidiano)
West Ham, Napoli na Inter Milan zote zinang'ang'ania kumsajili mchezaji wa Dynamo Kiev na mlinzi wa Ukraine Vitaliy Mykolenko, 21. (Sky Sport Italy)
Inter pia inamfuatilia kaw karibu kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 29. (La Gazetta dello Sport - in Italian)

Willian ajiunga rasmi na Arsenal
Arsenal imemsajili kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wa mchezaji huyo, 32, kukamilika.
The Blues ilitoa ofa yake mpya kwa mchezaji huyo lakini haikuwa tayari kufikia kile ambacho the Gunners imempa.
"Naamini ni mchezaji ambaye kweli anaweza kutufanyia mabadiliko makubwa," amesema kocha wa Arsenal Mikel Arteta.
Masharti ya usafiri kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19 huenda kukadidimiza uwezekano wa uhamisho wa kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek kuelekea ama Manchester United au Real Madrid, ambazo zite zina mnyatia mchezaji huyo, 23. (Fox Sports - in Dutch)
Uhamisho wa kiungo wa kati wa Schalke Weston McKennie kuelekea Hertha Berlin umeshindikana huku Wolves, Southampton na Leicester pia zikionesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, 21, -raia wa Marekani. (Bild - in German)
Preston inamatumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Charlton Athletic na Zimbabwe Macauley Bonne, 24, kwa pauni 500,000. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati Matty Longstaff ameanza kuwa huru mwezi huu
Kocha wa Newcastle Steve Bruce anafanya mazungumzo na Matty Longstaff kumshawishi mchezaji huyo, 20, kusaini mkataba mpya. Kiungo huyo wa kati wa Uingereza alianza kuwa huru mwezi huu baada ya mazungumzo juu ya mkataba wake kugonga mwamba. (Star)
Everton inakaribia kufikia makubaliano ya kumuuza kiungo wa kati Beni Baningime kwa mkopo katika klabu ya Ligi ya One Blackpool msimu ujao. (Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara
Washindi wa Ligi Kuu ya England Liverpool wamewasiliana na miamba wa Ujerumani Bayern Munich kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 29. (Bild, in German - subscription required).
Hata hivyo, Reds hawana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Vasco da Gama Mbrazil Talles Magno, licha ya tetesi zinazomhusisha kiungo huyo wa miaka 18- kuhamia Anfield. (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa wa Leicester City na England Ben Chilwel anang'ang'aniwa na United na Cheasea
United wako tayari kumenyana na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kusajili beki wa kushoto wa Leicester City na England Ben Chilwell, 23. (Mirror)
Kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak,27, anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusiana na hatima yake katika klabu hiyo japo Chelsea wanamtaka. (AS)
Napoli wako tayari kuafikiana na Everton kuhusu mkataba wa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Allan, 29. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Allan, 29
West Ham wanataka zaidi ya £80m kumuuza kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21, licha ya kiungo huyo kutakiwa na Chelsea. (Times - subscription required)
Na, Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller inasisitiza kuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, anayenyatiwa na Chelsea, ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo "chini ya hali fulani". (Kicker, via Standard)


0 comments:
Post a Comment