WAKATI Mabingwa wapya Chelsea na
Tottenham Hotspur tayari zishakata Tiketi 2 za Timu 4 Bora za EPL, LIGI KUU
ENGLAND, vita imebaki 2 zipi za mwisho zitaungana nao.
Vita hiyo sasa imebaki kwa
Liverpool, Man City na Arsenal ambayo itaamuliwa kwenye Mechi za mwisho za
Msimu hapo Jumapili Mei 21 baada Jana Man City na Arsenal zote kushinda Mechi
zao za Kiporo.
Jana Man City wakiwa kwao Etihad
waliitandika West Bromwich Albion 3-1 huku Bao zao zikipigwa na Gabriel Jesus,
Dakika ya 27, Kevin De Bruyne, 29, na Yaya Toure, 57.
Bao la WBA lilifungwa na Robson-Kanu
Dakika ya 87.
Kwenye Mechi yao ya mwisho hapo
Jumapili Ugenini na Watford, Man City wanahitaji Sare tu ili kujihakikishia
kuwemo 4 Bora.
Huko Emirates Jijini London, Arsenal
waliifunga Timu ambayo tayari ilishashushwa Daraja Sunderland Bao 2-0 zote
zikifungwa Kipindi cha Pili na Alexis Sanchez na kujiwekea matumaini ya kufuzu
4 Bora ikiwa mambo kadhaa yatatokea hapo Jumapili kwenye Mechi za mwisho kabisa
za Ligi.
Hapo Jumapili Arsenal kwanza inapaswa kuifunga Timu ya 7 Everton na pia kuomba Liverpool inafungwa na Middlesbrough ambayo tayari ishashuka Daraja.
Hapo Jumapili Arsenal kwanza inapaswa kuifunga Timu ya 7 Everton na pia kuomba Liverpool inafungwa na Middlesbrough ambayo tayari ishashuka Daraja.
Arsenal wapo Nafasi ya 5 wakiwa
Pointi 1 nyuma ya Liverpool ambao pia wana Goli 2 zaidi katika Tofauti ya
Magoli.
ARSENAL KUMALIZA 4 BORA - LAZIMA:
-Washinde na Liverpool ishindwe kuifunga Boro.
-Watoke Sare 0-0 au 1-1 na Liverpool kwa Bao 3 au zaidi.
-Wapate Sare ya Magoli ya 2-2 na Liverpool wafungwe 2-0 au Sare 3-3 na Liverpool wafungwe 3-1 na kadhalika.
-Washinde na Man City wafungwe na kubadili tofauti ya Magoli.na kuwa zaidi ya 5.
LIVERPOOL WATAMALIZA 4 BORA IKIWA:
-Watashinda au watapata matokeo yeyote bora kupita Arsenal
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumatatu Mei 15
Chelsea 4 Watford 3
Jumanne Mei 16
Arsenal 2 Sunderland 0
Manchester City 3 West Bromwich Albion 1
Jumatano Mei 17
2145 Southampton v Manchester United
Alhamisi Mei 18
2145 Leicester City v Tottenham Hotspur
Jumapili Mei 21
Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Everton
Burnley v West Ham United
Chelsea v Sunderland
Hull City v Tottenham Hotspur
Leicester City v Bournemouth
Liverpool v Middlesbrough
Manchester United v Crystal Palace
Southampton v Stoke City
Swansea City v West Bromwich Albion
Watford v Manchester City

0 comments:
Post a Comment