
Kocha wa Crystal Palace, Sam
Allardyce, amebwaga majanyanga ya kuendelea kuinoa timu hiyo akiwa kadumu kwa
miezi mitano tu kwenye klabu hiyo.
Big Sam alichukua mikoba ya kuinoa
timu hiyo toka kwa Alan Pardew mwezi Desemba mwaka jana akiwa na kazi ya
kuhakikisha timu inasalia katika ligi kuu ya nchini England, na akisaini
mkataba wa miaka miaka miwili na nusu.
Baada ya kuachana na klabu hiyo
iliyomaliza ligi katika nafasi ya 14, kocha huyo amesema hana mpango wa
kuchukua kazi nyingine katika mchezo wa soka.
"Ninataka kusafiri kutumia muda
wangu na familia yangu na wajukuu bila ya msukumo unaotoka na mchezo wa
soka," alisema kocha huyo
0 comments:
Post a Comment