Tuesday, May 16, 2017

Hakika ukizungumzia vilabu vyenye historia kubwa duniani huwezi kuacha vilabu vya Liverpool au Manchester United kutokana na ukongwe wao na historia ndani ya uwanja.
Sasa ukizungumzia klabu ya Liverpool imeingia katika rekodi mpya za soka na ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda mechi yao ugenini dhidi ya West Ham.
Liverpool imekuwa timu inayoongoza kwa kushinda mechi katika viwanja vingi vya ugenini, yaani Liverpool imeshinda michezo katika viwanja ambavyo sio vya kwao.
Majogoo hao wa London wamewahi kushinda katika viwanja 52 tofauti katika ligi kuu ya Uingereza rekodi ambayo hakuna timu katika ligi hiyo imeshawahi kushinda katika viwanja vingi kiasi hicho.
Wanaowafuatia Liverpool ni Manchester United na Arsenal ambao wote wana rekodi sawa kwani hadi sasa timu hizo zimeshinda katika viwanja 50 tofauti.
Baada ya Manchester United na Arsenal wanaofuatia ni mabingwa wa ligi kuu Uingereza klabu ya Chelsea ambao hadi sasa wameshinda katika viwanja 48 tofauti.
Katika hali ya kustaajabisha klabu ya Aston Villa
ambayo hata haipo ligi kuu iko sawa na Manchester City na Tottenham baada ya Aston Villa kushinda katika viwanja 46 sawa na vilabu hivyo viwili ambavyo viko top four ya ligi kuu.

0 comments:

Post a Comment