FAINALI UEFA EUROPA LIGI-LEO NI LEO MAN UNITED v AJAX HUKO SWEDEN!
- Details
- Created: Wednesday, 24 May 2017 05:18
FAINALI
24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden
Ajax Amsterdam v Manchester United
+++++++++++++++++++++++++++++++

Man
United walimaliza EPL, LIGI KUU ENGLAND, Nafasi ya 6 na hivyo kuikosa
Nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini Leo wakishinda wataungana
na Mabingwa wa England Chelsea, Tottenham na Man City kucheza Hatua ya
Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Liverpool,
ambao walimaliza Nafasi ya 4 kwenye EPL, wataanza Mechi za Mchujo na
wakifuzu ndio watatinga Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mechi
hii imekuja Siku 2 tu tangu Mlipuko wa Jijini Manchester ulioua Watu 22
na tukio hili litaifanya Man United kuvaa Utepe Mweusi Mkononi ikiwa ni
ishara ya Msiba.
Pia, Uwanjani, kabla Mechi kuanza, kila Mtu atasimama Dakika 1 kimya kuomboleza.
Ajax wanatinga kwenye Fainali ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1996.
Akiongelea
Fainali hii, Kocha wa Ajax Peter Bosz amesema Man United itapambana na
staili yao ya mashambulizi ya haraka na mfululizo.
Amedai hatabadili Mfumo huo licha ya kucheza na Man United ngumu na yenye uzoefu.
Kikosi cha Ajax kinategemewa kuwa na Vijana watupu na Mchezaji pekee mwenye Umri zaidi ya Miaka 25 ni Lasse Schone.
Man
United wataingia Mchezoni wakimkosa Beki wao Eric Bailly ambae alipewa
Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali na Velta Vigo na hivyo Kufungiwa.
Piam
Straika wao mahiri, Zlatan Ibrahimovic, Mwenyeji wa Sweden aliewafungia
Man United Bao 5 kwenye Mashindano haya, hayupo akijiuguza Goti lake.
Majeruhi wengine wa Man United ni Luke Shaw, Marcos Rojo na Ashley Young.
Ajax, ambao walimaliza Nafasi ya Pili kwenye Ligi ya kwao, watamkosa Fulbeki wao wa Kushoto Nick Viergever ambae yupo Kifungoni.
×××××××
JE WAJUA?
-MAN
UNITED wanasaka kujumuika na Ajax, Bayern Munich, Chelsea na Juventus
kwa kuwa Klabu pekee zilizonyakua Makombe yote ya UEFA huko Ulaya.
-Vikombe hivyo ni UEFA CHAMPIONZ LIGI, UEFA Cup Winners' Cup, UEFA Cup/UEFA EUROPA LIGI
×××××××
Ajax, chini ya Kocha Peter Bosz, wanasaka kutwaa Kombe lao la kwanza tangu Bosi huyo atue hapo Mwezi Mei Mwaka Jana.
Nae
Jose Mourinho, alianza kazi Man United mwanzoni mwa Msimu huu na tayari
ashatia Kabatini Ngao ya Jamii na EFL CUP huko England na sasa
analitaka Kombe hili ili Msimu ujao atinge UEFA CHAMPIONZ LIGI baada
kumaliza Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Hali za Timu
Ajax
ni Timu inayocheza kwa kushambulia kwa haraka kwa mfumo wa kaunta ataki
na Msimu huu kwenye Mashindano haya wamefunga Bao 24 wakati Man United
wamepachika 23 katika Mechi 14.
Ajax,
kikawaida, hutumia Mfumo wa 4-3-3 na Mtu 3 zao za Fowadi ni Kasper
Dolberg, Bertrand Traore, ambae ni wa Mkopo kutoka Chelsea, na Amin
Younes huku Fowadi wa Miaka 17, Justin Kluivert, Mwana wa Lejendari
Patrick Kluivert, mar kwa mara akiingizwa kuongeza nguvu kwenye Wingi.
Kwa
Man United, kumkosa Mkongwe Zlatan Ibrahimovic ambae ameumia na
aliepiga Bao 5 kwenye Mashindano haya ni pigo lakini yupo Kinda Marcus
Rashford ambae ni moto.
Pia kumkosa Ibrahimovic kunaweza kumfanya Jose Mourinho akabadili Mfumo kutoka ule wa jawaida yao wa 4-2-3-1.
Nguvu
kubwa ya Ajax ipo kwenye Kiungo chao na hasa Davy Klassen na Lasse
Schone na endapo Ander Herrera na Paul Pogba wataibuka juu yao, Difensi
ya Ajax, hasa Masentahafu Davinson Sanchez na Nick Viergever, si imara
kiasi hicho kwani huwa mchecheto kwenye presha na wao na Kipa wao Onana
hufanya makosa mengi kwenye hali hiyo.
Tiketi
Kila Timu imegawiwa Tiketi 9,500 kwa ajili ya kuuzia Mashabiki wao kwenye Uwanja huu wa Friends Arena unaopakia Watu 50,000.
Tiketi
zilizobaki zitauzwa Mtandaoni kwa Washabiki huko Sweden, Vyama vya Soka
vya Nchi husika, Washirika wa Kibiashara wa UEFA, Watangazi wa TV/Radio
wa Mechi hiyo na Kampuini maalum za kuhudumia Wateja.
Tiketi zote za Mechi hii zilikwisha kuuzwa Mawiki kabla Leo.
Refa
UEFA imemteua Refa
kutoka Slovenia Damir Skomina kuwa ndie atachezesha Fainali ya 2017 ya
UEFA EUROPA LIGI kati ya Ajax Amsterdam na Manchester United
itakayochezwa huko Stockholm, Sweden hapo Mei 24.
Uteuzi
huu huenda usimfurahishe Meneja wa Man United Jose Mourinho kwani
aliwahi kumbatukia Refa huyo na kumwita ‘dhaifu’ na ‘asiejua kitu’ baada
ya Refa huyo ‘kuidhulumu’ Chelsea Penati ya wazi Mwaka 2015 walipocheza
na Dynamo Kiev.
Refa Skomina pia ashawahi kuichezesha Man United Mwaka 2012 Uwanjani Old Trafford walipofungwa 2-1.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
AJAX: Onana; Tete, De Ligt, Sanchez, Veltman; Klaassen, Schone, Ziyech; Traore, Dolberg, Younes
MAN UNITED: Romero; Valencia, Blind, Jones, Darmian; Herrera, Fellaini, Pogba; Lingard, Rashford, Mkhitaryan
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
MAN UNITED: Romero; Valencia, Blind, Jones, Darmian; Herrera, Fellaini, Pogba; Lingard, Rashford, Mkhitaryan
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
UEFA EUROPA LIGI
WASHINDI WALIOPITA:
1971–72 Tottenham Hotspur
1972–73 Liverpool
1973–74 Feyenoord
1974–75 Borussia Mönchengladbach
1975–76 Liverpool
1976–77 Juventus
1977–78 PSV Eindhoven
1978–79 Borussia Mönchengladbach
1979–80 Eintracht Frankfurt
1980–81 Ipswich Town
1981–82 IFK Göteborg
1982–83 Anderlecht
1983–84 Tottenham Hotspur
1984–85 Real Madrid
1985–86 Real Madrid
1986–87 IFK Göteborg
1987–88 Bayer Leverkusen
1988–89 Napoli
1989–90 Juventus
1990–91 Internazionale
1991–92 Ajax
1992–93 Juventus
1993–94 Internazionale
1994–95 Parma
1995–96 Bayern Munich
1996–97 Schalke 04
1997–98 Internazionale
1998–99 Parma
1999–2000 Galatasaray
2000–01 Liverpool
2001–02 Feyenoord
2002–03 Porto
2003–04 Valencia
2004–05 CSKA Moscow
2005–06 Sevilla
2006–07 Sevilla
2007–08 Zenit Saint Petersburg
2008–09 Shakhtar Donetsk
(Mashindano yakabadilishwa na kuitwa UEFA EUROPA LIGI)
2009–10 Atlético Madrid
2010–11 Porto
2011–12 Atlético Madrid
2012–13 Chelsea
2013–14 Sevilla
2014–15 Sevilla
2015–16 Sevilla
0 comments:
Post a Comment