Monday, May 15, 2017


MANUNITED-MOU-CELEBRATES-WITH-TEAMJose Mourinho ametoboa Manchester United walishaamua kuipa kipau mbele UEFA EUROPA LIGI na si EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa sababu kuweka umuhimu kwa vyote viwili ilikuwa haiwezekani.
Jana Man United ilifungwa 2-1 na Tottenham huko White Hart Lane na kuiacha Tottenham ikipata hakika ya kubaki Nafasi ya Pili kwenye Ligi wakati Man United wakivunjiwa matumaini yao finyu ya kumaliza ndani ya 4 Bora.
Tayari Man United wana nafasi ya kucheza UEFA EUROPA LIGI Msimu ujao kwanza kwa kutwaa EFL CUP na pia wakimaliza Ligi Nafasi ya 5 au ya 6 ambayo hawawezi kuikosa.
Licha ya kuikosa 4 Bora ya EPL na hivyo kukosa nafasi ya kushiriki UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kutokana na Msimamo wa EPL, Man United wanayo nafasi ya kushiriki Mashindano hayo ikiwa tu wataifunga Ajax Amsterdam kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI itakayochezwa Jumatano Mei 24 huko Stockholm, Sweden.
Mourinho ameeleza: "Sikuchukizwa kutomaliza 4 Bora kwa sababu tuliamua. Watu wakisema tunacheza kamari kwa kutilia mkazo EUROPA LIGI..hatuchezi kamari. Hatukuchagua EUROPA, ilibidi iwe hivyo!"
Aliongeza: "Ningekuwa nao Ashley Young na Luke Shaw, Marcos Rojo, Zlatan Ibrahimovic, Tim Fosu-Mensah - ningekuwa nao hao, ningeweza kubadili Timu na kutilia mkazo kila Mechi! Lakini nina Wachezaji 14 au 15 tu. Siwezi kutilia mkazo kila Mechi. Haiwezekani ucheze kila baada Siku 3!"
Huku akiweka Jicho moja Fainali ya EUROPA LIGI, Mourinho ashaweka bayana atabadili Kikosi kwenye Mechi za Ligi za Jumatano dhidi ya Southampton na ile ya mwisho ya Ligi Jumapili na Crystal Palace.
Hata hivyo, Mourinho ameseka kwenye Vikosi vyake hataweka Chipukizi watupu tu kwa sababu anataka atoe upinzani.
Amesema: "Tumefungwa 2-0 na Arsenal lakini tulipigana. Tumepoteza 2-1 na Spurs tulipigana. Dhidi ya Southampton ni hivyo hivyo, ntabadili Timu lakini.itakuwa na ushindani. Blind hatacheza lakini Fellaini atacheza!

0 comments:

Post a Comment