Monday, May 15, 2017

LALIGA-2017-MBIOREAL MADRID Jana waliinyuka Sevilla 4-1 ndani ya Estadio Santiago Bernabeu Jijini Madrid na sasa kuhitaji Pointi 4 tu katika Mechi 2 walizobakiza ili kuwa Mabingwa wa LA LIGA huko Spain kwa mara ya kwanza tangu 2012.
Jana, Mabingwa Watetezi Barcelona, wakicheza Ugenini, waliiwasha Las Palmas 4-1 kwa Bao 3 za Neymar na moja la Luis Suarez na kuendelea kuongoza La Liga wakiwa Pointi sawa na Real na wao wako juu kwa ubora wa Magoli lakini wamebakisha Mechi 1 tu wakati Real wana Mechi 2.
Bao kwenye Mechi ya real na Sevilla zilifungwa na Nacho, Cristiano Ronaldo, Bao 2, na Toni Kroos.
Jumatano, Real wako Ugenini huko Estadio Balaidos kucheza Mechi yao ya Kiporo na Celta Vigo na utashindi kwao utawaweka Pointi 3 mbele ya BarcaLALIGA-MEI15 huku Mechi zikibaki 1 kwa kila Timu.
LA LIGA 
Ratiba/Matokeo:
Raundi ya 37
 **Saa za Bongo
Jumamosi Mei 13
Espanyol 0 Valencia 1 
Osasuna 2 Granada 1 
Jumapili Mei 14
Alaves 3 Celta Vigo 1 
Athletic Club 1 Leganes 1 
Real Betis 1 Atletico Madrid 1 
Eibar 0 Sporting Gijon 1
Las Palmas 1 Barcelona 4 
Real Madrid 4 Sevilla 1 
Real Sociedad 2 Malaga 2 
Villarreal 0 Deportivo 0 
Jumatano Mei 17
22:00 Celta Vigo v Real Madrid 
Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
21:45 Granada v Espanyol 
Jumamosi Mei 20
18:00 Deportivo v Las Palmas 
18:00 Sporting Gijon v Real Betis 
18:00 Leganes v Alaves 
Jumapili Mei 21
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club 
17:45 Celta Vigo v Real Sociedad 
17:45 Sevilla v Osasuna 
17:45 Valencia v Villarreal 
21:00 Barcelona v Eibar 
21:00 Malaga v Real Madrid

0 comments:

Post a Comment